Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Sekondari 2025 (KCSE) nchini Kenya umeingia siku yake ya pili.

Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC) lilisema kuwa maandalizi yote yako sawa ili kuhakikisha mchakato wa uwazi, baada ya kufanya tamrini siku ya Ijumaa.

‘Mipango ya tathmini ya kitaifa ya mwaka huu imekamilika. Tunatarajia wadau wote wakiwemo watahiniwa, walimu, wazazi, wasimamizi washirikiane ili kufanikisha mitihani hiyo.” Rais wa Kenya William Ruto amesema.

Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC Davind Njengere alisema kuwa wanafunzi mwaka huu, jumla ya watahiniwa 996,078 wamesajiliwa kufanya mitihani ya KCSE katika zaidi ya vituo 10,000 kote nchini.

Wanafunzi wengine 1,298,089 watafanya mitihani ya Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) inayotarajiwa kuanza wiki ijayo huku 1,130,669 watafanya Tathmini ya Elimu ya Shule ya Vijana ya Kenya (KJSEA).

Waziri wa Elimu Julius Ogamba pia alisisitiza kujitolea kwa serikali kwa mchakato wa mtihani wa kuaminika na wa haki.

“Serikali imejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa anafanya mtihani wake katika mazingira salama na yanayofaa,” alisema, akiongeza kuwa uratibu kati ya KNEC, Wizara ya Elimu, na taasisi za usalama utadumishwa katika kipindi chote cha mtihani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *