
Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali usiku wa kuamkia leo. Hapa Ujerumani Bayer Leverkusen wakiwa nyumbani Bay Arena walichapwa 7-2 na mabingwa watetezi wa kombe hili Paris Saint German, vigogo wengine wa Ujerumani Borrusia Dortmund wao waliwacharaza Copenhagen ya Denmark 4-2.
Barcelona yaUhispania waliinyeshea mvua ya magoli 6-1 Olympiacos ya Ufaransa huku Wahipania wengine Atletico Madrid wakiangukia pua kwa kuchapwa 4-0 na Arsenal ya England.
Hii leo, mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watawakaribisha Club Brudge ya Ubelgiji huku Real Madrid wakimenyana na kibibi cha Turin Juventus. Mechi hizi zitachezwa majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.