Makumi ya watu wameripotiwa kufariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria baada y...

Makumi ya watu wameripotiwa kufariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria baada ya gari hilo kuteleza kutoka barabarani na kuanguka, na kumwaga mafuta.

Wanakijiji walikimbilia eneo la ajali kuchota mafuta kutoka kwa lori lililopinduka lakini likapuka ghafla na kuwaka moto mkubwa uliowateketeza.

Takriban watu 30 waliripotiwa kufariki, huku wengine wasiopungua 40 wakipata majeraha ya moto viwango tofauti.

Moto huo mkali ulitewaketeza waathiriwa wengi kiasi cha kutotambulika, na waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya karibu kwa matibabu.

Ajali zinazohusisha magari ya mafuta hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, licha ya onyo kutolewa kuhusu ya hatari ya kuteka mafuta yaliyomwagika.
#Chanzobbcswahili
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *