Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetahadharisha uwepo na mwenendo wa Kimbunga CHENGE katika Bahari ya Hindi, Kaskazini Mashariki mwa Kisiwa cha Madagascar umbali wa takribani kilometa 2400 kutoka Mashariki mwa pwani ya Mtwara.
Kimbunga “CHENGE” kilianza kujitengeneza Mashariki mwa Bahari ya Hindi Oktoba17, 2025 na kuendelea kusalia katika eneo hilo huku kikiimarika.
Taarifa ya Mamlaka hayo imesema kuwa uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa kwa sasa inaonesha kuwa Kimbunga “CHENGE” kinatarajiwa kuelekea Magharibi zaidi mwa Bahari ya Hindi ulipo ukanda wa pwani ya nchi katika kipindi cha siku nne hadi tano (kati Oktiba 26 hadi 27,2025) huku kikipungua nguvu yake.
“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga “CHENGE” na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi,” imesema taarifa hiyo.
Kufuatia hali hiyo mamlaka hayo imeshauri watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka TMA pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.
#StarTvUpdate