Iran iko tayari kutoa jibu kali kwa uchokozi wowote endapo utafanywa dhidi yake katika siku zijazo. Ameyasema hayo Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye ametaharisha kuwa Iran “itaachilia moto wa kuzimu dhidi ya adui.”

Meja Jenerali Mohammad Pakpour ameeleza hayo jana alipokutana na kuzungumza mjini Tehran na Qasim al Araji Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq.

Kamanda Mku wa jeshi la IRGC ameashiria uvamizi wa siku 12 uliofanywa na Israel na Marekani dhidi ya Iran mwezi Juni mwaka huu na kutahadharisha kuwa maadui wanataka kudhoofisha umoja wa nchi za kikanda.

“Utawala wa Kizayuni ulitaka kuvuruga  mshikamano wa kitaifa wa Iran kupitia kuwauwa makamanda na kufanya hujuma, lakini kwa hekima ya Kiongozi Muadhamu na umakini wa wananchi, njama hiyo ilisambaratishwa,” amesema Kamanda Pakpour. 

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameongeza kuwa na hapa ninamnukuu: “Adui alidhani kuwa uwezo wetu wa makombora ungepungua katika siku za mwanzo za vita, lakini tulichukau hatua kwa nguvu na kwa usahihi, na kuteketeza kwa usahihi shabaha tulizozikusudia”, mwisho wa kunukuu. 

Meja jenerali Muhammad Pakpour amepongeza juhudi za Iraq za kuyadhibiti makundi yaliyo dhidi ya Iran wakati wa vita vya siku 12 na kutaka kutekelezwa kikamilifu makubaliano ya usalama ya pande mbili na kuanzishwa kamati ya nyanjani ya kufuatilia maeneo ya mipakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *