Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema ufanisi mkubwa unaoonekana katika sekta ya bandari nchini ni ushahidi wa hatua za kimkakati zilizochukuliwa katika kuimarisha miundombinu na usimamizi wa bandari.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika Kinyerezi, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Makonda amesema maboresho hayo yameongeza uwezo wa bandari kushughulikia mizigo kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa takwimu alizozitaja, bandari ya Dar es Salaam imeongeza uwezo wake kutoka tani milioni 18 hadi milioni 27 kwa mwaka, bandari ya Mtwara kutoka tani 590,000 hadi milioni 2.5, na bandari ya Tanga kutoka tani 809,000 hadi milioni 1.3.
✍ Mwandishi Wetu
#AzamTVUpdates