Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wake wa kuunda tume mbalimbali, un…Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wake wa kuunda tume mbalimbali, un…

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wake wa kuunda tume mbalimbali, unalenga kuongeza ushirikishwaji wa wananchi na kutenda haki dhidi ya changamoto na kero zinazowakabili.

Amelifafanua hilo, akirejea tume alizowahi kuziunda kutatua changamoto za wananchi, ikiwemo ya haki jinai, kuangalia mifumo ya kodi na ile ya kutatua kero zinazowakabili wakazi wa Ngorongoro.

Hata hivyo, kupitia tume ya haki jinai ambayo tayari ilishawasilisha ripoti yake na utekelezwaji umeanza kufanyika, kumeshuhudiwa mifumo ya haki jinai ikibadilika na kuimarisha utendaji wa haki.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Oktoba 22, 2025 alipozungumza na wananchi wa Ilala jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Amesema Serikali yake imeunda tume mbalimbali kutatua changamoto na kero za wananchi, zikilenga kuwashirikisha wananchi na kutenda haki kwao, kwani ndio wanaotoa mamlaka kwa watawala.

“Tume zote hizi zimekwenda kwa wananchi kuwasikiliza na kuchukua maoni yao, huo ndio utawala bora ndugu zangu, hakuna anayejua kila kitu.

“Ukitaka kuendesha nchi kwa amani lazima uwashirikishe wenye nchi na ndio demokrasia, tunafanya kazi kwa ajili ya watu naona na wao watu ndio wenye mpini katika kuendesha nchi hii na sio watawala,” amesema Dkt Samia.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *