Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kujenga daraja jipya la Jangwani lenye urefu wa mita 390 pamoja na soko kubwa la kisasa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo, ndani ya miaka mitano ijayo iwapo chama chake kitapewa ridhaa ya kuunda serikali.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Viwanja vya Kecha, Kinyerezi, Ilala, Dkt. Samia amesema maandalizi yote ya ujenzi wa daraja hilo yamekamilika, na litawezesha kupunguza msongamano, kurahisisha usafiri na kuimarisha shughuli za kiuchumi jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa ilani ya CCM 2025/2030 pia imepanga kujenga madaraja mengine ikiwemo la Mzinga, na flyovers katika maeneo ya Tabata, Buguruni na Fire.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *