Sekretarieti ya WHO FCTC imewaonya serikali na umma kuwa sekta ya tumbaku inaongeza juhudi zake za kuingilia kazi ya Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ya Mabadiliko ya Tabianchi- (COP), chombo kinachofanya maamuzi ya mkataba huo, kwa lengo la kudhoofisha hatua za kimataifa za kudhibiti matumizi ya tumbaku.

WHO FCTC ni mkataba wa kwanza uliowahi kujadiliwa chini ya mwamvuli wa WHO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani), na ni mojawapo ya mikataba ya Umoja wa Mataifa iliyopokelewa kwa haraka zaidi na kwa upana mkubwa. Jumla ya Nchi Wanachama 183 zimejiunga na Mkataba huu, ambao ulianza kutekelezwa miaka 20 iliyopita.

Mkutano wa Kumi na Moja wa COP, ambao utafanyika kuanzia tarehe 17 hadi 22 Novemba huko Geneva, Uswizi, utawakutanisha nchi,wanachama wa mkataba huu ili kufanya maamuzi muhimu kwa utekelezaji wa malengo ya WHO FCTC, yakiwemo majadiliano kuhusu hatua za kuzuia uraibu wa nikotini, na kulinda mazingira pamoja na afya ya binadamu, miongoni mwa mengine.

Mkutano wa Nchi Wanachama wa Itifaki ya kuondoa biashara haramu ya bidhaa za Tumbaku (MOP) utafanyika Geneva, Uswizi kuanzia tarehe 24 hadi 26 Novemba. Mkutano huu ni chombo kinachosimamia utekelezaji wa Itifaki hiyo ya kimataifa ambayo ilianza kutumika mwaka 2018 na sasa ina Nchi Wanachama 71. Katika MOP, Nchi Wanachama zitajadili hatua mbalimbali za kuimarisha Itifaki hiyo na nafasi yake katika kuondoa biashara haramu ya bidhaa za tumbaku.

Hili si suala la ushawishi wa kawaida, ni mkakati uliokusudiwa kuharibu maelewano na kudhoofisha hatua za kutekeleza mkataba huu, amesema Andrew Black, Kaimu Mkuu wa Sekretarieti ya WHO FCTC.

“Uingiliaji wa sekta ya tumbaku ni mojawapo ya vizingiti vikubwa zaidi katika utekelezaji wa Mkataba huu. Sekretarieti imezihimiza vikali Nchi Wanachama, asasi za kiraia na wadau wengine wanaounga mkono udhibiti wa tumbaku kuwa macho dhidi ya mbinu na upotoshaji wa sekta ya tumbaku. Serikali zina wajibu chini ya WHO FCTC wa kutekeleza ipasavyo Kifungu cha 5.3, ambacho kinataka kulinda sera za afya ya umma dhidi ya maslahi ya kibiashara na mengine ya sekta ya tumbaku.”

Ushahidi kutoka kwa wadau huru wa asasi za kiraia, zikiwemo zile zilizo waangalizi wa Mkutano wa COP, unaonesha kuwa uingiliaji wa sekta ya tumbaku unajumuisha:

·        Kukamata kisiasa (political capture)-  Kujaribu kuweka watu wanaoiunga mkono sekta ya tumbaku katika ujumbe wa taifa au kuwa na ushawishi juu ya uteuzi wao ili kuathiri majadiliano.

·        Makundi ya mbele na sauti huru-  Mashirika yanayofadhiliwa na sekta ya tumbaku yanayojitokeza kama makundi ya biashara, sayansi au watumiaji ili kushawishi ujumbe wa taifa.

·        Kupotosha sayansi-  Kufadhili au kukuza tafiti zenye upotoshaji ili kuleta mashaka kuhusu hatua za udhibiti wa tumbaku ambazo tayari zimeonyesha mafanikio.

·        Kauli za kiuchumi-  Kuweka shinikizo kwa wizara za fedha na biashara kwa madai yasiyo sahihi kuhusu ajira, kilimo na mapato ya kodi.

·        Upenyaji wa upatikanaji-  Kujaribu kupata hadhi ya kuwa waangalizi au kushiriki katika matukio yanayohusiana na COP ili kuathiri majadiliano.

Mbinu hizi zinafanana na zile zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Kielezo cha Uingiliaji wa Sekta ya Tumbaku Duniani (Global Tobacco Industry Interference Index), ambayo inaonesha jinsi sekta hii inavyojaribu kuathiri sera za umma duniani kote.

Sekretarieti ya WHO FCTC inazitaka nchi wanachama kufanya yafuatayo

·        Kutekeleza kikamilifu Kifungu cha 5.3 cha WHO FCTC na Miongozo yake ya utekelezaji, ili kulinda Sehemu zote za Serikali dhidi ya ushawishi wa sekta ya tumbaku.

·        Kulinda Mkutano wa COP dhidi ya maslahi ya kibiashara ya sekta ya tumbaku, kwa mujibu wa Lengo la 3.1.3 la mkakati wa kimataifa wa kukuza udhibiti wa tumbaku-  Kuendeleza maendeleo endelevu kupitia utekelezaji wa WHO FCTC 2019-2030, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya ujumbe wa nchi.

·        Kuhakikisha kwamba wajumbe wa COP na MOP hawajumuishi watu kutoka sekta ya tumbaku au walio na uhusiano nayo.

·        Kukataa ufadhili au ushirikiano wowote unaohusiana na sekta ya tumbaku, ikiwa ni pamoja na kwa shughuli za COP, MOP au ujumbe wa taifa.

·        Kutoa elimu kwa wizara zisizo za afya kuhusu mbinu za sekta ya tumbaku na wajibu wa utekelezaji wa Kifungu cha 5.3.

·        Kutumia zana zilizopo za ufuatiliaji kama vile Global Tobacco Industry Interference Index ili kubaini uingiliaji. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *