Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetoa zaidi ya shilingi bilioni 527.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi 13 ya barabara, madaraja na mizani katika Mkoa wa Tabora.

Meneja wa TANROADS mkoani humo, Mhandisi Raphael Mlimaji amesema miradi saba kati ya hiyo imekamilika kwa asilimia 92.5 ikiwemo ujenzi wa barabara za Nyahua–Chaya, Usesula–Komanga, na Komanga–Kasinde, pamoja na maboresho ya uwanja wa ndege wa Tabora. Miradi mingine sita yenye thamani ya shilingi bilioni 39.6 inaendelea katika hatua mbalimbali za ujenzi na usanifu, ikiwemo barabara za Puge–Ziba–Choma na Tabora–Ulyankulu.

Mhandisi Mlimaji amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji, kuongeza ufanisi katika biashara, kukuza utalii na uchumi wa Tabora.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *