Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limefanya maboresho yatakayoongeza ufanisi na kuhakikisha msimu wa korosho wa 2025/2026 unakuwa na tija kubwa kwa wakulima na wadau wa sekta hiyo.
Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji wa Biashara wa TMX, Justa Martine, amesema taasisi hiyo imeimarisha mifumo ya biashara na miundombinu ya TEHAMA ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuongeza uwazi wa bei na kuwezesha uuzaji wa korosho kupitia mfumo rasmi wa soko hilo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi