
Nchini Sudan Kusini, kumekuwa na mshtuko na maswali mengi kuhusu kufukuzwa kwa raia wa Sudan Kusini wanaoishi katika nchi jirani ya Sudan. Zaidi ya wakimbizi milioni moja wakiwemo raia 800,000 wa Sudan Kusini wamemiminika nchini Sudan Kusini tangu kuanza kwa vita nchini Sudan mwezi Aprili 2023.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Raia wengi wa Sudan Kusini wamesalia nchini Sudan, hasa mjini Khartoum, ambako kwa sasa wanakabiliwa na kampeni ya kuwarejesha makwao kwa lazima, ambayo imekuwa ikiendelea kwa wiki moja iliyopita. Akina mama wamefukuzwa Sudan Kusini bila watoto wao.
Siku ya Jumanne, Oktoba 21, watoto 71 waliunganishwa tena na mama zao. Hii ni afueni kwa akina mama walio kuwa wakijiuliza maswali kuhus watoto zao. Walifukuzwa Oktoba 13 na polisi wa Sudan baada ya kufanyika kwa ukaguzi mitaani na manyumbani kwao kwa vibali vya kuishi nchini Sudan, walilazimika kuwatelekeza watoto wao. Hivi ndivyo, kwa mujibu wa taarifa zetu, karibu watu 300 wamefukuzwa kutoka Sudan, kupitia kivuko cha mpaka cha Joda, tangu wiki iliyopita.
Watoto waachwa nchini Sudan
Mamlaka katika Kaunti ya Renk, iliyoko kaskazini-mashariki mwa Sudan Kusini, imesisitiza kuwa watoto waliotelekezwa warejeshwe. Walitangaza siku ya Jumanne kwamba wamefanikiwa kuwapata watoto 71 huko Khartoum na kuwaunganisha na mama zao, na wanatoa wito kwa uhamishaji wowote wa siku zijazo kutekelezwa kwa heshima kubwa kwa familia.
Kampeni kubwa inayolenga wageni na wakimbizi wasio na vibali halali vya ukaazi inaendelea nchini Sudan. Kulingana na takwimu rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani iliyonukuliwa na vyombo vya habari vya mtandaoni Sudan Tribune, karibu wageni 20,000 walilengwa na hatua hiyo.