Takribani watu 46 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa kwa ajali iliyohususha magari manne katika Barabara ya Ka...

Takribani watu 46 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa kwa ajali iliyohususha magari manne katika Barabara ya Kampala na mji wa Gulu.

Ajali hiyo iliyotokea Jumatano asubuhi,katika Kijiji cha Kitaleba, ilihusisha mabasi mawili, Lori na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser, kwa mujibu wa ripoti ya awali ya polisi.

Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka kutokana na baadhi ya abiria kujeruhiwa vibaya.

“Inaelezwa kuwa basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa likilipita lori na basi jingine lililokuwa likielekea Kampala lilikuwa likiipita gari ndogo ya Toyota Land Cruiser, lakini lilishindwa kufanya hivyo kwani tayari basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa limekaribia’’. Taarifa ya polisi imeeleza.

#StarTvUpdate
#chanzobbcswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *