
Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana Antoine Semenyo, 25, msimu wa uhamisho wa wachezaji Januari mwakani. (i Paper – usajili unahitajika)
Kiungo wa kati wa Nottingham Forest na England Elliot Anderson, 22, ananyatiwa na Manchester United. (Mirror)
Mshambulizi wa Brazil Endrick yuko tayari kuondoka Real Madrid mwezi Januari, huku wawakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 wakiwa mbioni kukamilisha uhamisho wake wa malipo. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 23, yuko katika hatua za awali za kujadili kandarasi mpya na klabu ya Aston Villa. (Sky Sports)
Villa pia wako tayari kumpa kiungo wa kati wa Scotland John McGinn, 31, mkataba mpya. (Fabrizio Romano)
Tottenham inaripotiwa kuwa tayari kuwasilisha ofa ya takribani euro milioni 60 kumsajili mshambuliaji wa Al-Ahli na England Ivan Toney, 29. (Fichajes – kwa Kihispania)
West Ham ina mpango wa kuwasajili walau wachezaji watatu – mshambuliaji, kiungo wa kati na beki – mnamo Januari katika juhudi ya kuimarisha nafasi yao ya kushinda taji. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Reuters
Barcelona bado wanadaiwa £138m za ada ya uhamisho, ikiwa ni pamoja na £36.5m za klabu ya Leeds United kwa ajili ya winga wa Brazil Raphinha, 28, na £12m za Manchester City kwa ajili ya mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, 25. (Talk Sport)
Meneja wa Manchester United Ruben Amorim ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 37 msimu ujao. (Star)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi