
Raia watano wa Ufaransa, wakiwemo wanne kutoka Bouches-du-Rhône, wenye umri wa kati ya miaka 70 na 75, wamefariki siku ya Jumanne, Oktoba 21, katika ajali ya barabarani nchini Togo, shirika la misaada lililoandaa safari hiyo limeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Miongoni mwa wahasiriwa, watatu wanatoka La Ciotat, katibu wa shirika la Lions Clubs la jiji hilo ameliambia shirika la habari la AFP, ambaye aliomba kutambuliwa tu kwa jina lake la kwanza, Aurélien.
Kutoka Togo, walitakiwa kusafiri hadi nchi jirani ya Benin kuzindua wodi ya wazazi inayofadhiliwa na shirika hilo, amesema, wakati basi lililokuwa limebeba abiria “lipotumbukia kwenye mtaro” kutokana na “kupasuka kwa tairi.”
Serikali ya Togo imethibitisha katika taarifa yake vifo vya watu watano, bila kutaja uraia wao, na kuripoti kujeruhiwa wanane katika “ajali mbaya ya barabarani” siku ya Jumanne huko Yomaboua, katikati mwa nchi.