Chanzo cha kijeshi nchini Sudan kimesema leo Jumatano kwamba wanamgambo wa RSF wameushambulia tena kwa droni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum kwa siku ya pili mfululizo. Chanzo hicho kimesema vikosi vya anga vya jeshi viliyakabili mashambulizi hayo, ingawa RSF haijadai kuhusika.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Sudan ilikuwa imetangaza kufunguliwa kwa uwanja huo leo baada ya maandalizi ya kiufundi kukamilika, lakini kufuatia mashambulizi mapya, haijulikani kama shughuli zitaanza kama ilivyopangwa.

Jana Jumanne, milipuko kadhaa ilisikika karibu na uwanja huo, wakati mkuu wa jeshi, Abdel Fattah al-Burhan, akiahidi “kuangamiza uasi wa RSF.”

Vita kati ya jeshi na RSF, vinavyoendelea tangu Aprili 2023, vimeua maelfu ya watu na kuwafanya takriban milioni 12 kuyahama makazi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *