VIWANJANI: “malengo aliyonayo Azam siyo malengo aliyonayo KMKM”
Mchambuzi wa soka Philip Nkini amesema mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Azam FC dhidi ya KMKM anaamini utakuwa mgumu kutokana na malengo ya kila timu kwenye michuano hiyo.
Huku naye mchambuzi Ayubu Hinjo ameongeza kuwa anaamini wachezaji wa KMKM wataenda katika mchezo huo kwa kujituma ili kujihakikishia ushindi huku Azam FC anatakiwa kuboresha eneo la ulinzi na ushambuliaji.
Imeandikwa na @davidkyamani
#Viwanjani