
Taarifa hiyo imeongeza kuwa uporaji huo umefanyika kuanzia mwezi Mei mwaka huu wakati M23 ilipochukua udhibiti wa mgodi wa Twangiza uliopo Kivu Kusini na kwamba baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Twangiza Mining walihusika katika vitendo hivyo.
Kundi hilo la waasi wa M23 linaloungwa mkono na Rwanda halijazungumzia chochote juu ya taarifa hiyo, lakini kampuni ya Twangiza Mining imesema inajiandaa kuwasilisha malalamiko rasmi kwa mamlaka za Kongo na kwa makundi ya wapatanishi wa kimataifa, ikiwashutumu waasi hao wa M23 kwa kuwafukuza wakaazi, kubomoa makanisa na kutumia wataalam wa Rwanda kutanua eneo la uchimbaji.