Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ilizinduliwa rasmi mkoani Manyara Oktoba 11,2025 ambapo uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama iliambatana na uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa ukaguzi wa vyombo vya moto na utoaji wa stika za usalama barabarani.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Rehema Buruhani Shaibu amefafanua namna ya kujisajili katika mfumo huo, ambao unatarajiwa kuondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika ukaguzi wa magari kwa kutumia stika za karatasi, na badala yake kurahisisha huduma kwa njia ya Kidigitali.

@imjenalpha
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *