CAFCC: Golikipa wa Azam FC, Aishi Manula anasema kesho watu wasishangae kama watamuona ameshika bendera na anakimbia uwanjani baada ya timu yake kufuzu hatua ya makundi.
Manula anasema Azam FC ndio timu anayoipenda, ndio timu iliyomlea na yeye anatamani sana kuiona ikitinga hatua ya makundi kesho.
Azam FC itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya KMKM katika mchezo wa mkondo wa pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Mechi hiyo itapigwa saa 11:00 jioni LIVE #AzamSports2HD
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#CAFCC #AzamFC