Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeboresha kwa kiwango kikubwa miundombinu yake ya TEHAMA kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa…Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeboresha kwa kiwango kikubwa miundombinu yake ya TEHAMA kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa…

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeboresha kwa kiwango kikubwa miundombinu yake ya TEHAMA kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET), hatua itakayoongeza ufanisi katika ufundishaji, ujifunzaji na utoaji wa huduma za kimtandao chuoni hapo.

Akizungumza mbele ya wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea chuo hicho kuona maendeleo ya utekelezaji wa mradi, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Anangisye, amesema kupitia Mradi wa HEET, Chuo kina mpango wa mahususi wa kukuza ushirikiano kati ya Chuo na Sekta Binafsi katika eneo la ubunifu na biashara ya teknolojia.

Prof Anangisye amesema mradi wa HEET una mchango mkubwa kwa Chuo na Taifa, Pia unaendana sambamba na Mpango mkakati wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam wa mwaka 2021/2022 – 2030/2031 na ni hatua muhimu katika kuzalisha wahitimu wabunifu, waadilifu, na wenye uwezo wa kuongoza nchi kuelekea uchumi wa kati na wa ngazi ya juu.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amepongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa usimamizi mzuri wa mradi huo, akisema majengo yanayojengwa yanaonyesha kiwango kikubwa cha utaalamu na ubunifu.

Aidha Katika maboresho ya mitaala, UDSM imefanyia mapitio mitaala 250 ili yalingane na mahitaji ya soko la ajira, ikijumuisha muda wa mafunzo ya vitendo na ujuzi wa wahitimu. Huku Watumishi 29 wakifadhiliwa kusoma Uzamivu na Umahiri katika vyuo vikuu vya kimataifa, ambapo asilimia 30 ni wanawake.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *