#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, linamshikilia mtuhumiwa mmoja mwenye umri wa miaka 46, mkazi wa Kamala, Wilaya ya Kigoma, Mkoa wa Kigoma kwa tuhumu ya mauaji ya mtoto wake, aitwaye Salimu Nusura, miaka 12, baada ya kumjeruhi kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili akimwadhibu kwa tuhuma ya kuiba fedha kiasi cha Tsh.700,000.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani upelelezi utakapokamilika.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kutumia njia ya ukatili dhidi ya watoto wanapowahoji watoto wanaokinzana na sheria, bali watumie njia ya kisheria au mazungumzo kwa kuwafikisha watoto hao sehemu sahihi ikiwemo Ustawi wa jamii au Dawati la Jinsia na Watoto ili wahojiwe kwa mujibu wa sheria.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.