#HABARI: Marekani imetangaza vikwazo vipya vikubwa kwa sekta ya mafuta ya Urusi.

Vikwazo hivyo vinalenga kumpelekea Rais Vladimir Putin, kukubali kufanya mazungumzo ya amani na hatimaye kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Vikwazo hivyo dhidi ya kampuni kubwa za mafuta za Rosneft na Lukoil, vinafuatia miezi kadhaa ya miito kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ya kumtaka Trump, aiwekee Urusi vikwazo vikubwa zaidi katika sekta ya mafuta ya nchi hiyo.

Sekta hiyo ya mafuta ni muhimu katika kuendesha uchumi wa Urusi, na imeuwezesha utawala wa Putin kuendelea na vita dhidi ya Ukraine licha ya kutengwa pakubwa kimataifa.

Marekani imetangaza vikwazo hivyo wakati ambapo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte yuko mjini Washington kwa mazungumzo na Trump.

Haya yanafanyika wakati ambapo Urusi imeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Ukraine kwa usiku wa pili mfululizo.

Shambulizi la usiku wa kuamkia leo, limepelekea watu 4 kujeruhiwa na majengo katika wilaya kadhaa kuharibiwa mjini Kyiv.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *