#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuf ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kuwezesha na kuhamasisha upatikanaji wa nishati bora na salama kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji ili Watanzania watumie nishati safi na salama nchini.
Mhe. Jamila ametoa pongezi hizo wakati akifungua mafunzo ya elimu ya matumizi ya nishati safi kwa makundi maalum iliyofanyika mkoani Katavi.
Mbali na REA Mhe. Jamila amewapongeza pia TAMAVITA (Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania) kwa kushirikiana na REA katika uhamasishaji na kukubali kupewa mafunzo hayo kutoka REA ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.