#HABARI: Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Zambia kupitia Tunduma (TAZA) umefikia asilimia 83.45 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 2026 na hivyo kufungua soko jipya la biashara ya umeme barani Afrika.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo katika eneo la Iganjo, Mbeya, amesema mradi wa TAZA ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa utaiunganisha Tanzania na Nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool) na pia kuimarisha muunganiko wa ukanda wa Mashariki mwa Afrika (East Africa Power Pool).
“Nimshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati. Kupitia mradi huu tutaimarisha biashara ya kuuza na kununua umeme kati ya nchi za Mashariki mwa Afrika na zile zilizopo Kusini mwa Afrika”. Amesema Dkt. Mataragio
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.