#HABARI: Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amewasili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya muendelezo wa kesi ya Uhaini inayomkabili.

Ikumbukwe hapo jana, Mahakama hiyo ilikubaliana na pingamizi la tatu lililowasilishwa na Lissu na kukataa kupokea flashi na memori kadi kama Ushahidi, kutokana na shahidi huyo kutokakuwa na sifa ya kuwasilisha ushahidi huo mahakamani, kwa kuwa yeye ni mtaalamu wa picha mnato na sio mjongeo, na aliyepaswa kiwasilisha ushahidi huo kwa mujibu wa sheria ni mtaalamu wa kisayansi wa makosa ya mtandaoni.

Mahakama iliamua kuwa shahidi wa tatu wa upande wa Mashtaka, Inspekta wa Polisi Samwel Kaaya (39), si mtaalamu wa uchambuzi wa video bali ni mtaalamu wa upigaji picha za kawaida ambazo ni mnato.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Dustan Nduguru, kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo.

Lissu aliwasilisha hoja nne kupinga upokelewaji wa vielelezo hivyo, akidai kuwa shahidi huyo hana sifa stahiki za kuwasilisha ushahidi huo mahakamani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *