#HABARI: Treni ya Mwendokasi (SGR) imeripotiwa kupata ajali baada ya kuacha njia, katika eneo la Ruvu mkoani Pwani asubuhi ya leo Oktoba 23, 2025 ikiwa inatokea jijini Dar es Salaam kuelekea Dodoma.
Kwa mujibu wa abiria wawili waliozungumza, wamesema hawajamuona mtu yeyote aliyejeruhiwa ila ni hofu tu iliyowapata wachache.
Msemaji wa Shirika la Reli (TRC) Fredy Mwanjala amethibitisha kupokea taarifa za ajali hiyo; “tumepokea hizo taarifa za Treni kupata ajali na kwa kuwa ndio kwanza tumezipata kwa sasa Mkurugenzi Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara wote tunaelekea eneo la tukio na tutatoa taarifa baadae baada ya kufanya tathmini ya kina na wataalamu.”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.