#HABARI: Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Nandagala, Ruangwa mkoani Lindi na kuagiza kituo hicho kianze kazi ifikapo Novemba 1, mwaka huu.

Mhe. Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Frank Chonya, kuhakikisha samani zinawekwa katika kituo hicho ili kiweze kutumika kwa kutoa huduma kwa Wakazi wa Wilaya ya Ruangwa.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, John Imori, amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 164 kilitengwa kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi cha Daraja C, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu ameagiza kituo hicho kijengwe kwa mfumo wa Force Account na fedha nyingine zijenge nyumba za Maafisa wa Polisi.

Ujenzi wa kituo hicho ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 194.3 umefikia asilimia 95 za utekelezaji, kukamilika kwake kutawezesha wananchi Katika Vijiji 32 kwenye kata 8 za Wilaya ya Ruangwa kupata huduma.

Kadhalika, Mhe. Majaliwa ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana ya Liuguru ambapo aliwaeleza wanafunzi hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeongeza fursa kwa watoto wa kike kupata elimu nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *