HASHEEM IBWE ASEMA RAHA ZIPO CHAMAZI: “Sisi tunakwenda kesho uwanjani tukiwa tumetanguliwa magoli mawili”
Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe anasema pamoja na timu yao kuwa na mtaji wa magoli mawili waliyoyapata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya KMKM, lakini kesho wataingia uwanjani kama wanaanza upya.
Ibwe anasema wamewatengeneza wachezaji waone kama mechi haijaanza ili kuongeza ari na kuweza kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Ibwe anasema kesho milango ya dimba la Azam Complex, itafunguliwa saa nne asubuhi na kuwaalikwa mashabiki wote ikiwemo wale wanaokosa raha kwenye timu zao kwenda kuitazama mechi hiyo na tayari ‘tajiri’ amenunua tiketi zote ili watu wakatazame mechi.
Mechi hiyo itapigwa saa 11:00 jioni LIVE #AzamSports2HD
#AzamFC #HasheemIbwe #Ibwe