Ikiwa zimesalia siku sita kuelekea uchaguzi mkuu Tanzania unaofanyika oktoba 29.2025, viongozi wa dini , wazee wakimila na vyama vya siasa wameshiriki katika kongamano la amani lililofanyika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga likiwa limeandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo.
Katika kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Muheza Ayoub Sebabili amewataka viongozi wa dini kuongeza juhudi Katika kuelimisha wauimini umuhimu wa kulinda na kuthamini amani na mshikamano kwa kuepuka hamasa za aina yoyote zitakazopelekea uvunjifu wa amani huku akisema kua kamati ya usalama wilaya hiyo imejipanga vizuri Katika kulinda raia na Mali zao.
Kwa upande wa viongozi hao wamesema watahakikisha wanafikisha elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa amani kuanzia sasa mpaka uchaguzi utakapokamilika na wameahidi kuwasistiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi.
#StarTvUpdates
