Tahadhari hiyo imetolewa baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia nishati ya Atomiki kuelezea hofu ya uwezekano wa ‘matumizi mapya ya nguvu’ ikiwa juhudi za kidiplomasia na Tehran zitagonga mwamba.

Mnamo katikati ya Juni, Israel ilifanya mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya Iran, na kusababisha vita ambapo Iran ilijibu kwa makombora na droni. 

Wakati wa mzozo huo wa Israel na Iran, vita hivyo vilivyodumu kwa siku 12, Israel ilishambulia vituo vya kijeshi na vya nyuklia vya Iran huku Marekani ikijiunga baadaye kwa kushambulia vinu vikuu vya nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *