Jeshi la Nigeria lawaua zaidi ya wanamgambo 50 wa Boko Haram
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limewaua wanamgambo zaidi ya 50 wa kundi la Boko Haram baada ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kutekelezwa na kundi hilo dhidi ya kambi za kijeshi katika kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.