Oktoba ni mwezi maalumu kwa ajili ya kujenga ufahamu kuhusu saratani ya matiti. Ni wakati wa kuwakumbuka waathirika wa aina hii ya saratani, lakini pia kuthibitisha tena dhamira yetu ya kimataifa ya upatikanaji sawa wa huduma na maisha bora kwa wote.