Ushindi huo kwa Liverpool umefikisha mwisho msururu wao wa kupoteza mechi nne mfululizo katika mashindano yote ila ulitiliwa doa na majeraha kwa wachezaji wao muhimu Alexander Isak na Jeremie Frimpong.

Kiungo mbunifu wa timu ya taifa ya Ujerumani Florian Wirtz aling’aa katika mechi hiyo kwa kutoa pasi muhimu zilizopelekea kupatikana kwa mabao ya Cody Gakpo na Dominik Szoboszlai.

Kwengineko mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich walikuwa na kazi rahisi uwanjani kwao Allianz Arena walipowalaza Club Brugge mabao 4-0 Lennart Karl, Harry Kane, Luis Diaz na Nicholas Jackson wakiwa wafungaji wa mabao hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *