Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro, Profesa Mussa Assad, amesema changamoto kubwa kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu siyo kukosa nafasi katika uchumi, bali ni kukosa ujuzi wa vitendo unaowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema serikali na sekta binafsi zinapaswa kushirikiana kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu, ili kuwajengea stadi zinazohitajika kwenye soko la ajira.
Akizungumza katika kongamano la kitaaluma la kujadili utekelezaji wa Uchumi Jumuishi kuelekea Dira 2050, Profesa Assad pia amesema uchumi wa Tanzania umeimarika kwa wastani wa asilimia 6 katika miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hali inayodhihirisha maendeleo na uimara wa uchumi wa taifa.
✍ Theresia Mwanga
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates