Makumi ya watu wameripotiwa kufariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria. Ripoti zinasema tukio hilo limetokea katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria baada ya gari hilo kuteleza kutoka barabarani na kuanguka, na kumwaga mafuta.

Wanakijiji walikimbilia eneo la ajali kuchota mafuta kutoka kwenye lori lililopinduka lakini likapuka ghafla na kuwaka moto mkubwa uliowateketeza.

Takriban watu 30 wameripotiwa kufariki dunia, huku wengine wasiopungua 40 wakipata majeraha ya moto kwa viwango tofauti.

Moto huo mkali ulitewaketeza waathiriwa wengi kiasi cha kutotambulika, na waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya karibu kwa ajili ya matibabu.

Ajali zinazohusisha magari ya mafuta hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, licha ya onyo kutolewa kuhusu ya hatari ya kuteka mafuta yaliyomwagika.

Limekuwa jambo la kawaida huko Nigeria ambapo watu wengi huhatarisha maisha yao kwa kukimbilia malori yanayopinduka ili kuchota mafuta hasa ukizingatia kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo tangu serikali ilipositisha mpango wake wenye gharama kubwa wa kufadhili ruzuku ya gesi.

Januari mwaka huu wauu wasiopungua 86 waliaga dunia katika Jimbo la Niger, nchini Nigeria katika tukio la mlipuko mkubwa wa lori la mafuta.

Kadhalika Oktoba mwaka jana watu karibu 200 walipoteza maisha yao katika jimbo la Jigawa la kaskazini mwa Nigeria katika mlipuko uliosababishwa la ajali ya lori la mafuta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *