Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekabidhiwa rasmi majengo ya kikosi cha mafunzo kwa Mbwa Nusa, yaliyotolewa na Shirika la Kimataifa la African Wildlife Foundation (AWF) jijini Arusha.
Lengo ni kuimarisha ulinzi wa rasilimali za wanyamapori na kudhibiti usafirishaji haramu wa nyara kupitia mipaka na viwanja vya ndege.
Tangu kuanzishwa mwaka 2015, kikosi hicho kimesaidia kukamatwa kwa watuhumiwa 99 wa biashara haramu ya nyara, kikitumia mbwa maalum kunusa bidhaa kama meno ya tembo na ngozi za wanyama pori.
✍ Ramadhani Mvungi
#AzamTVUpdates