Vikwazo hivyo vinavyolenga kumpelekea Rais Vladimir Putin kukubali kufanya mazungumzo ya amani na hatimaye kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Vikwazo hivyo dhidi ya kampuni kubwa za mafuta za Rosneft na Lukoil vinafuatia miezi kadhaa ya miito kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ya kumtaka Trump aiwekee urusi vikwazo vikubwa zaidi katika sekta ya mafuta ya nchi hiyo.

Sekta hiyo ya mafuta ni muhimu katika kuendesha uchumi wa Urusi na imeuwezesha utawala wa Putin kuendelea na vita dhidi ya Ukraine licha ya kutengwa pakubwa kimataifa.

Marekani imetangaza vikwazo hivyo wakati ambapo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte yuko mjini Washington kwa mazungumzo na Trump.

Haya yanafanyika wakati ambapo urusi imeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Ukraine kwa usiku wa pili mfululizo.

Shambulizi la usiku wa kuamkia leo limepelekea watu 4 kujeruhiwa na majengo katika wilaya kadhaa kuharibiwa mjini Kyiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *