MBEYA CITY vs JKT TANZANIA: “Tunajua kabisa haitakuwa mechi rahisi”
Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema mchezo wao wa kesho wa NBC Premier League dhidi ya Mbeya City utakuwa mchezo mgumu kutokana na maandalizi yaliyofanywa na timu zote mbili.
Kocha huyo ameongeza kuwa wanamheshimu mpinzani wao kutokana na ubora wake katika michezo yake aliyocheza ila na wao pia wamejipanga kukabiliana naye na kila mchezaji yuko tayari kwa mchezo.
Kwa upande wake mchezaji Gamba Matiko amesema wao kama wachezaji wamejipanga vizuri kwa mchezo huo na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwauga mkono.
Mechi hiyo itapigwa kesho Ijumaa saa 10:00 jioni #AzamSports1HD.
Imeandikwa na @davidkyamani
Mhariri: @allymufti_tz
#AzamSports1HD #JKTTanzania #NBCPremierLeague