
Mfalme Charles III, amekuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa la England kufanya ibada ya hadharani na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Leo XIV, ambayo haijawahi kufanyika kwa miaka 500 iliyopita. Ibada hiyo ilioongozwa na Papa huko Vatican.
Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 76 pamoja na mke wake Malkia Camilla, walijiunga na Papa Leo katika Kanisa Dogo la Sistine kwa Ibada ya Misa ya dakika 30 wakichanganya tamaduni za Kikatoliki na Kianglikana
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa mfalme anayetawala Uingereza kusali hadharani na Papa tangu Mfalme Henry VIII alipoachana na Kanisa Katoliki la Roma mnamo mwaka wa 1534.
Utengano huo ulichochewa na hatua ya papa wa wakati huo kukataa kubatilisha ndoa ya Henry ili aweze kuoa mwanamke mwengine.