
Tchiroma Bakary amewataka Wacameroon kuandamana, endapo Baraza la Katiba litatangaza kile alichokiita ‘matokeo potofu na yaliyochakachuliwa’ kwenye uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkali.
Rais wa sasa Paul Biya mwenye umri wa miaka 92 anasaka muhula wa nane ili kurefusha utawala wake wa miaka 43, baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 12na ambao umekumbwa na madai ya udanganyifu.
Tchiroma anadai kwamba kulingana na takwimu alizokusanya mwenyewe, alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 54.8 dhidi ya Biya aliyedai alipata asilimia 31.4.
Tangu wiki iliyopita, wafuasi wa Tchiroma wamekuwa wakilalamika na kujitokeza mitaani kudai ushindi wa mgombea wao.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu ya Oktoba 27.