Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa serikali ijayo chini ya CCM itaendelea kusimamia maendeleo ya watu kama msingi mkuu wa kujenga taifa lenye utu, usawa na ustawi kwa wote.
Akihutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Dkt. Samia amesema dira ya CCM imejikita katika kuendeleza utu wa Mtanzania kwa kuhakikisha kila raia anapata huduma muhimu na fursa za kujikwamua kiuchumi.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates