“Matangazo hayo ya matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 12, 2025, yatafanyika siku ya Jumatatu, Oktoba 27, saa tano asubuhi,” kulingana na taarifa iliyotolewa na Baraza la urais Jumatano jioni.

“Tujitokeze kwa ajili ya ukombozi na kudai ushindi wetu,” Tchiroma alisema kupitia njia ya video katika mtandao wa Facebook, akiwataka wanaomuunga mkono kuwa “kitu kimoja katika suala la amani na kwa mapenzi ya nchi yetu.”

Chama cha RDPC cha Biya kimepinga madai ya ushindi wa Tchiroma na kutaja hatua hiyo kama “ulaghai” na “uwizi usiokubalika katika nchi inayofuata sheria”, wakisema katika taarifa kuwa “wanasubiri kwa hamu matokeo rasmi”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *