Rubio amesema hatua zilizochukuliwa na bunge la Israel pamoja na ghasia za walowezi kwenye eneo hilo, zinatishia mkataba wa amani wa Gaza.

Mnamo Jumatano, wabunge wa Israel walipitisha miswada miwili ya kuuzingira Ukingo wa Magharibi.

Hatua hiyo imejiri wiki moja tu tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango wa Rais Donald Trump wa usitishaji vita na unaolenga kumaliza kabisa mzozo kati ya Israel na Hamas, ambao umedumu sasa kwa miaka miwili.

Huko the Hague, Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, imesema ni sharti Israel iliruhusu Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina Gaza (UNRWA), kuendelea na shughuli zake za kiutu.

Rais wa mahakama hiyo Yuji Iwasawa amesema Israel ina jukumu la kukubali na kuweka mazingira mazuri ya mashirika ya misaada kufanya shughuli zake. Israel haijairuhusu UNRWA kuingiza misaada tangu mwezi Machi, ila shirika hilo linaendelea kuendesha vituo vya matibabu, huduma za usafi na shule kwa watoto Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *