Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) imezindua rasmi mradi maalum wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda bioanuwai nchini.

Mradi huo utatumia mbinu chanya na jumuishi katika kulinda misitu na kuongeza manufaa ya kiuchumi yatokanayo na uhifadhi wa rasilimali hizo muhimu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, amesema mradi huo utaanza kutekelezwa katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, huku serikali ikipanga kuupanua katika mikoa mingine nchini.

#AzamTVUPdates
✍ Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *