Shirika la Reli Tanzania (TRC), imesema chanzo cha ajali ya treni ya umeme (SGR),Shirika la Reli Tanzania (TRC), imesema chanzo cha ajali ya treni ya umeme (SGR),

Shirika la Reli Tanzania (TRC), imesema chanzo cha ajali ya treni ya umeme (SGR),
iliyokuwa ikisafiri kutoka Stesheni ya Magufuli jijini Dar es Salaam kwenda Dodoma ni hitilafu za kiuendeshaji.

Ajali hiyo imetokea leo Alhamisi asubuhi, Oktoba 23, 2025 katika eneo la Ruvu, mkoani Pwani.

Taarifa ya Shirika hilo, imesema kuwa ajali hiyo imesababisha mabehewa matatu kuacha njia.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa taarifa za awali zinaonyeja hakuna tulio la kifo.

“Timu ya wataalamu ikiongonzwa na Katibu Mkuu Uchukuzi, Mkurugenzi Mkuu TRC, vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya TRC inaendelea na uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikishahuduma zetu zinarejea haraka,’ imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Shirika hilo limewaomba radhi wateja wake Kwa usumbufu uliojitokeza.

#startvupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *