Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema ajali ya treni ya EMU iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma imesababishwa na hitilafu za kiuendeshaji.

Taarifa ya TRC kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wake mkuu imesema ajali hiyo imetokea kituo cha Ruvu majira ya saa 2.00 asubuhi leo Oktoba 23, 2025.

“Timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu Uchukuzi, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya TRC, inaendelea na uchunguzi wa kina na kuhakikisha huduma zinarejea,” imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa, taarifa za awali ni kwamba hakuna vifo.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *