Treni ya Mwendokasi ya Reli ya Kisasa (SGR) iliyokuwa ikielekea Dodoma kutoka Dar es Salaam imepata ajali leo Alhamisi, Oktoba 23, 2025, majira ya asubuhi katika eneo la Ruvu, mkoani Pwani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya treni hiyo kuacha njia (reli) na kuanguka, wakati ikiendelea na safari yake ya kawaida.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, hakuna vifo vilivyoripotiwa hadi sasa juhudi za kuwapata viongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kueleza kwa kina chanzo na hatua zinazochukuliwa kuhusu ajali hiyo zinaendelea.
✍ Mariam Songoro
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates