Akitangaza vikwazo hivyo Trump amesema mazungumzo yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kumaliza vita vya Ukraine ‘hayaendi popote.’

Kwa miezi mingi, Trumpamejizuia kuiwekea Urusi vikwazo, lakini uvumilivu wake ulifikia mwisho baada ya mipango ya kukutana na Putin huko Budapest kugonga mwamba.

”Jambo pekee ninaloweza kusema ni kwamba kila ninapozungumza na Vladimir, tunakuwa na mazungumzo mazuri. Na kisha hayaendi popote. Lakini tizama, anapigana vita. Yuko kwenye vita vikali vya pande mbili. Na ndivyo vita vilivyo. Lakini ninaweza kusema muda umewadia. Muda umewadia wa kufikia makubaliano. Watu wengi wanakufa,’ amesema Trump’

Umoja wa Ulaya pia ulitangaza vikwazo vipya kuishinikiza Urusi kumaliza vita vyake Ukraine ambavyo vimedumu kwa miaka mitatu na nusu sasa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyamepongeza vikwazo hivyo vipya vya Marekani na Umoja wa Ulaya, akivitaja kuwa ujumbe thabiti na unaohitajika zaidi kuishinikiza Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *