Umoja wa Ulaya utarejesha uhusiano wake wa kibiashara wa upendeleo na Israel hatua kwa hatua kwa kisingizio cha kutekelezwa usitishaji unaolegalega wa mapigano huko Gaza.
Umoja wa Ulaya ambao huko nyuma ulipungiza uhusiano wake wa kibiashara wa upendeleo na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mashinikizo ya waliowengi duniani ambao walitaka kulaania Israel na kuchukuliiwa hatua kutokana na mauaji ya kimbari ya Gaza, mara hii umeanzisha tena uhusiano huo kwa kisingizo cha usitishaji vita unaolegalega katika Ukanda wa Gaza. Kuhusu suala hilo, Kaja Kallas, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametangaza kwamba jitihada za kusimamisha biashara ya upendeleo kati EU na utawala wa Kizayuni na kuwawekea vikwazo shakhsia ambao wanahusika na kuchochea mapigano huko Gaza, zitasitishwa.
Kwa utaratibu huu, Brussels kwa mara nyingine tena imekosolewa kufuatia kuondolewa vikwazo ambavyo Umoja wa Ulaya ulikuwa umeviweka dhidi ya utawala wa Kizayuni. Hii ni katika hali ambayo Shirika la Haki za Binadamu la Ulaya na Mediterania hivi karibuni liliutaka Umoja wa Ulaya uendelee kuuwekea mashinikizo utawala wa Kizayuni ili uache kukiuka haki za msingi za Wapalestina. Shirika hilo aidha lilisisitiza katika taarifa yake kuwa kuweka vikwazo na kufuta mikataba ya kibiashara na Israel ni muhimu ili kukomesha mauaji ya kimbari huko Palestina.
Hata hivyo, Umoja wa Ulaya, katika hatua inayokinzana pakubwa na sera zake za nje na nara na shaari zake za uwongo, unasisitiza kuanzisha tena uhusiano na Israel kama hapo awali.
EU ambayo katika miongo kadhaa ya karibuni imefanya kila iwezalo kujiarifisha kama mchezaji mkuu katika sera za kimataifa na upande unaoheshimu masuala kama haki za binadamu, demokrasia na uhuru katika miezi ya hivi karibuni, kufuatia siasa za chuki na zisizo za kibinadamu za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wanaoishi Gaza, ulidai kuwa umeiwekea vikwazo Israel na kukata uhusiano wake na utawala huo ghasibu. Uamuzi huo ulichukuliwa na maafisa wa Ulaya kutokana na mashinikizo ya maoni ya umma katika nchi za bara hilo na kwengineko duniani.

Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, wananchi wa nchi mbalimbali za Ulaya walifanya maandamano ya kupinga siasa za Ulaya za kuihami na kuipatia Israel misaada ya kifedha na silaha wakizitaka serikali za nchii za Ulaya kukata uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi na utawala huo katili. Matokeo ya mashinikizo hayo yalikuwa kulegeza kamba viongozi wa Ulaya, huku baadhi ya serikali za nchi za bara hilo, kama Uhispania, zikitangaza kuwa zitalitambua rasmi taifa la Palestina na kuvunja uhusiano wao wa kiuchumi na utawala wa Kizayuni. Hata hivyo kilichopuuzwa ni mienendo ya kinafiki, kindumakuwili na kinzani ya muungano huo. Kwani kwa upande mmoja, Umoja wa Ulaya unatangaza nara za kutetea haki za binadamu na uadilifu, na kwa upande mwingine, kivitendo, bado unaendeleza uhusiano wa karibu na Israel kwa ajili ya maslahi yake ya kiuchumi na kisiasa.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, migongano hiyo haiishi katika uhusiano wa Ulaya na Israel. Mara nyingi, Umoja wa Ulaya pia umepitisha na kutumia sera za kinafiiki na kindumakuwili katika kushughulikia masuala ya nchi nyingine. Kwa mfano, katika nchi nyingi za Kiafrika, Wazungu, walifanya na wanaendelea kufanya unyonyaji na mauaji mabaya zaidi katika nchi za bara hilo licha ya kujionyesha kuwa watetezi wa haki za binadamu na demokrasia. Sera hizi za kinafiki sio tu zimepelekea kuongezeka ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu na taasisi za kimataifa, lakini pia zimetilia shaka vikali uhalali wa Umoja wa Ulaya katika uga wa kimataifa.
Sasa, wakati Brussels imeamua kuondoa vikwazo dhidi ya Israel na imetupiilia mbali msimamo wake kuhusu utawala huo katili, Claudio Francavilla, mkurugenzi wa Shirika la Haki za Kibinadamu la Euro-Mediterranean, kanda ya Ulaya ametangaza rasmi kwamba kilichobadilika hadi sasa ni ukubwa na ukali wa jinai za kutisha za Israel huko Gaza; lakini ukaliaji haramu na wa kimabavu, jinai za ubaguzi wa rangi, kulazimishwa watu kuyahama makazi yao, mateso na ukandamizaji wa Wapalestina vinaendelea bila kusita.

Msimamo mpya wa Ulaya, yaani mabadiliko ya sera na kurejesha mahusiano ya kibiashara ya upendeleo na Israel, umeibua maswali mazito kuhusu uaminifu na malengo ya kweli ya Umoja wa Ulaya. Hali hii, hususan kuhusu Israel na Palestina, inaonyesha kuwa Umoja wa Ulaya unafuata maslahi yake badala ya kuzingatia kanuni za kibinadamu na haki za binadamu; mtazamo ambao unapingana kabisa na kauli mbiu na nara tupu za Ulaya za kuunga mkono haki za binadamu na kudhihirisha udhaifu wa umoja huo katika kukabiliana na migogoro ya binadamu na ya kisiasa. Sera hizi za kinafiki na kindumakuwili, kwa hakika zinaakisi uayari na uzandiki unaofichua sura halisi ya Umoja wa Ulaya na nchi za Magharibi kwa ujumla.